Back to Hymns and Songs

Song · Kiswahili

Nitatangaza

Verse 1

Nitatangaza matendo yako dunia yote ikujue Adonai hakuna mungu kama wewe. Umetukuka dunia yote umenitoa mbali sana, umehifadhi roho yangu nikusifu naimba sifa zako Emanueli nakuabudu,

Chorus

Nitaimba sifa zako Hosanna, walio uhai wakujue umbali umenileta Ebeneza, wewe ndiye Mungu. Nitaimba sifa zako Hosanna, walio uhai wakujue umbali umenileta Ebeneza, wewe ni Mungu.*2

Verse 2

Umenitoa mbali sana, Jina lako Jiree limeninasua Kwenye magonjwa mikosi pia, hata umasikini umevunja laana zote, umenipa heshima uhai bure. Mwamba imara hutingiziki, wewe ndiye Mungu

Verse 3

Umeokoa nafsi yangu, umejitwika hayaa nipate heshima Uhai wako ukatoa niishi, Yahweh nakuabudu nitaimba sifa zako, nitatangaza wema wako Hosanna wenye mataifa wakujue, wema na mwaminifu