Verse 1
Yesu unipendaye kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye mwovu akinijia. Yafiche ubavuni mwako maisha yangu; Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.
Verse 2
Ngome nyingine sina; nategemea kwako, Usinitupe Bwana, nipe neema yako, Ninakuamania, kuniweshesha; Shari wanikingia, vitani wanitosha.
Verse 3
Nakutaka mpaji, vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, utanijazi vyako; Nao waangukao wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, uongoze vipofu.
Verse 4
Bwana umeniosha moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha yapatikana kwako; Kwako Bwana naona kisima cha uzima; Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.
